image

Asia na Pasifiki

Afisi ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa inafanya kazi ili kuleta maendeleo, kuboresha na kuhakikisha kuna rasilimali za kutosha kwenye eneo zima.

Latest

Learn how plastic gets into Asian rivers

Resource

All you need to know about air pollution.

Get Involved

COVID-19 Updates from UNEP.

Learn More
Changamoto
Asia ya Pasifiki ndilo eneo linalokua kwa kasi kote ulimwenguni. 

Ukuaji huu wa uchumi, licha ya kuinua watu wengi kutoka kwa umaskini, umesababisha uharibifu mkubwa kwa mazingira, uharibifu ambao unaathiri binadamu vibaya. Changamoto yetu ni jinsi ya kudumisha na kukuza maendeleo ya karne mbili zilizopita kwa njia endelevu.

Soma zaidi • Kuhusu afisi hii
 • Miradi ya Kanda

Afisi ya eneo la Asia na Pasifiki ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa inapatikana Bangkok. Tuna afisi ya kitaifa kule Beijing na afisi ya ukanda kule Samoa, pia tunapatikana katika nchi zingine kupitia miradi ya kitaifa ikiwa ni pamoja na Programu ya UN-REDD na Mradi wa Umaskini na Mazingira. Afisi ya eneo la Asia na Pasifiki pia ni mwenyeji wa sekretarieti za Mashirika yafuatayo:

 • Mpango wa Kushughulikia Bahari katika Eneo la Asia Mashariki
 • Mtandao Unaofuatilia Udhibiti wa Asidi katika Eneo la Asia Mashariki
 • Jukwaa la Mazingira na Maendeleo la Eneo la Asia ya Pasifiki
 • Mtandao wa Mabadiliko wa Eneo la Asia ya Pasifiki
 • Ubia wa Hewa Safi wa Eneo la Asia ya Pasifiki
 • Shirika Linaloratibu Bahari za Asia Mashariki
 • Mkataba wa Maafikiano Kuhusu Kobe kati ya Bahari Hindi na Asia ya Kusini Mashariki
 • Jukwaa la Kanda Kuhusu Mazingira na Afya
 • Afisi ya Mabadiliko Nchi ya Mtandao wa Asia ya Kusini Mashariki
 • Jukwaa Endelevu la Mchele
 • Ubia wa Kimataifa wa Matumbawe ya Maeneo ya Bahari wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa
roap

Afisi ya eneo la Asia na Pasifiki ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa

2nd Floor, Block A, UN Building
Rajdamnern Avenue, Bangkok 10200

Katika eneo la Asia Pasifiki, Afisi ya eneo la Asia na Pasifiki ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa inafanya kazi katika ngazi ya kanda, ukanda, na ya kitaifa kuwezesha majadiliano na ubia ili kushughulikia mazingira vizuri.

Soma zaidi kuhusu miradi yetu