Kwa nini Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa ni muhimu?

Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UN Environment) ndilo linaongoza duniani kwa kuweka ajenda za kimataifa za mazingira, linawezesha utekelezaji wa maendeleo endelevu kwenye nyanja ya mazingira kupitia kwa  mfumo wa Umoja wa Mataifa, na hufanya kazi kama mtetezi mkuu wa mazingira duniani.

Dhima yetu ni  kuongoza na kuwezesha ushirikiano  katika utunzaji wa mazingira kwa kuhimiza, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuimarisha hali yao ya maisha bila kuathiri yale ya vizazi vijavyo.

Tukiwa na Makao Makuu Nairobi, Kenya tunafanya kazi kupitia kwenye idara zetu na pia kupitia katika afisi zetu za kimaeneo na kupitia kwa mtandao unaokua wa vituo bora kabisa vinavyoshirikiana. Pia sisi ni wenyeji wa maafikiano kadhaa kuhusu mazingira, masekretatiat na mashirika mashirika mbalimbali yanayoleta pamoja mawakala wa uratibu. Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa huongozwa na Mkurugenzi mwendeshaji. 

Huwa tunagawa kazi yetu kwa makundi makuu saba: tabia nchi, majanga na mizozo, ushughulikiaji wa mfumo wa ikolojia, udhibiti wa mazingira, kemikali na taka, utumizi mzuri wa rasilimali, na mazingira yanayokaguliwa. Kwa kazi yetu yote, sisi hujitolea kwa dhati kudumisha uendelevu. 

Wanaowezesha kazi yetu ni wabia wanaotufadhili na kuendeleza dhima yetu. Sisi hutegemea mchango kutoka kwa wahisani kwa asili mia 95.

Kila mwaka sisi huheshimu na kujivunia watu binafsi na taasisi zinazofanya kazi ya kipekee kwa ajili ya mazingira.

Sisi pia ni wenyeji wa sekritarieti  za mashirika ya kila aina yenye mikataba mbalimbali ya kimazingira na mashirika ya utafiti, hali inayotuwezesha kuleta pamoja mataifa na jamii za kimazingira ili kukabiliana na changamoto  sugu zilizopo. Hii ni pamoja na:

  • Mapatano ya bayolojia anuai 
  • Mapatano kuhusu Biashara ya Kimataifa ya Viumbe Vilivyo Karibu Kuangamia vya Fauna ya Porini na Flora
  • Mapatano ya Minamata kuhusu Zebaki
  • Mapatano ya Basel, Rotterdam na Stockholm
  • Mapatano ya Vienna ya kutunza ozoni na Itifaki ya Montreal
  • Mapatano kuhusu viumbe vihamaji
  • Mapatano ya Carpathian
  •  Mapatano ya Bamako
  •  Mapatano ya Tehran