Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UN Environment) ndilo linaongoza duniani kwa kuweka ajenda za kimataifa za mazingira, linawezesha utekelezaji wa maendeleo endelevu kwenye nyanja ya mazingira kupitia kwa mfumo wa Umoja wa Mataifa, na hufanya kazi kama mtetezi mkuu wa mazingira duniani.
Dhima yetu ni kuongoza na kuwezesha ushirikiano katika utunzaji wa mazingira kwa kuhimiza, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuimarisha hali yao ya maisha bila kuathiri yale ya vizazi vijavyo.
Tukiwa na Makao Makuu Nairobi, Kenya tunafanya kazi kupitia kwenye idara zetu na pia kupitia katika afisi zetu za kimaeneo na kupitia kwa mtandao unaokua wa vituo bora kabisa vinavyoshirikiana. Pia sisi ni wenyeji wa maafikiano kadhaa kuhusu mazingira, masekretatiat na mashirika mashirika mbalimbali yanayoleta pamoja mawakala wa uratibu. Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa huongozwa na Mkurugenzi mwendeshaji.
Huwa tunagawa kazi yetu kwa makundi makuu saba: tabia nchi, majanga na mizozo, ushughulikiaji wa mfumo wa ikolojia, udhibiti wa mazingira, kemikali na taka, utumizi mzuri wa rasilimali, na mazingira yanayokaguliwa. Kwa kazi yetu yote, sisi hujitolea kwa dhati kudumisha uendelevu.
Wanaowezesha kazi yetu ni wabia wanaotufadhili na kuendeleza dhima yetu. Sisi hutegemea mchango kutoka kwa wahisani kwa asili mia 95.